Tuesday, February 14, 2012

JEMBE SUAREZ OMBA RADHI


Mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez na meneja wake Kenny Dalglish wameomba radhi kufuatia Suarez kukataa kumpa mkono Patrice Evra kabla ya mechi siku ya Jumamosi.
"Nimezungumza na meneja baada ya mchezo wa Old Trafford na nimetambua kuwa nilikosea," amesema Suarez katika taarifa iliyotolewa na klabu hiyo.
"Kila mmoja wetu ana jukumu la kuiwakilisha klabu hii katika mtindo unaofaa," alisema siku ya Jumapili.
"Jukumu hilo pia ninalo mimi kama meneja wa Liverpool.
"Nilipozungumza kwenye TV baada ya mchezo sikuwa nafahamu kilichotokea, lakini pia siku fanya kile kinachotarajiwa kufanywa na meneja wa Liverpool katika mahojiano, na ningependa kuomba radhi kwa hilo."
Manchester United ilitoa taarifa ikisema: "Manchester United inawashukuru Liverpool kwa kuomba radhi kufuatia matukio ya siku ya Jumamosi. Kila mmoja Old Trafford anataka kuondokana na jambo hilo.
"Historia ya vilabu vyetu viwili ni ya mafanikio na uhasama katika soka la Uingereza. Hilo ndio liwe lengo letu siku za usoni kwa mashabiki wanaozipenda timu hizi."
Suarez alifungiwa kucheza mechi nane kwa kumbagua na kumtusi Evra wakati wa mchezo wa ligi mwezi Oktoba mwaka jana.
Kukataa kwake kumpa mkono Evra siku ya Jumamosi kulichangia kuufanya mchezo huo kuwa wa vuta nikuvute ambapo United walishinda 2

UWOYA CHELSEA DAMU YANGA DAMU



Mwanamaigizo wa kiwango cha juu hapa Bongo ametoa maoni yake juu ya kufanya vibaya kwa klabu ya Chelsea ambayo ndio timu ya nje anayoishabikia.

Uwoya ambaye ni mke wa mwanasoka Hamad Ndikumana anayekipiga katika ligi kuu ya nchini Cyprus amesema msimu huu Chelsea wamemuangusha sana lakini anaamini hiki ni kipindi cha mpito tu ila mambo yatarudi kuwa mazuri darajani


 "Msimu timu yetu imekuwa haipo vizuri kabisa, me napenda soka na Chelsea ndio ninayopenda kwa nje ya Tanzania. Naamini timu yetu inapitia katika mabadiliko ila mambo yataanza kukaa sawa na tutarudi kwenye chati tena. Nashukuru sasa hivi mchezaji wangu kipenzi Micheal Essien amerudi hivyo ataongeza uimara katika kikosi chetu."


Pamoja na kuizungumzia Chelsea pia mwanadada huyo amesema kwa hapa nchini anaipenda sana Yanga na anaamini wanajangwani watamfuta machozi wikiendi hii watakapokutana na Zamalek ya Misri.
"Nina uhakika Zamalek lazima wachezee kichapo wikiendi hii. Timu yetu ipo vizuri na sasa tuna mshawasha na spirit ya kufanya vizuri kwa sababu tupo katika kipindi cha kusherehekea miaka 77 tangu Yanga aianzishwe.





" Rafiki yangu kipenzi Jerry Tegete naamini hatoniangusha na atatupia goli kadhaa kwenye goli la waarabu siku hiyo. Mimi nitaenda uwanjani kama kawaida kwenda kuwasapoti watoto wa Jangwani na naamini tutashinda."by japhet

UZINDUZI WA STUDI MPYA ZA B HITS NDANI YA MAISHA CLUB ilukuwa hivi?

AY na FA

Izzo B


Cyrill


Nyomi

Hemed

Juxx
duuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu ilukuwa noma sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.

SINTA KUKUTANA TENA NA NATURE NDAN YA MOVIE MOJA NA JUMA NATURE "STAKI DEM"


Movie star wa bongo mrembo SINTAH ametangaza kwamba mwanzo mwa march mwaka huu, wanaanza kushoot movie na mpenzi wake wa zamani msanii JUMA NATURE, movie ambayo itazungumzia maisha yao ya kimapenzi kabla ya kuachana zaidi ya miaka 10 iliyopita, inaitwa ‘SITAKI DEM” jina ambalo ni la track ya Nature aliitoa wakati alipoachana na SINTAH.

Sintah amesema “siku hizi mambo ya ugomvi yamepitwa na wakati japo ilikua shida sana mwanzoni wakati tunauanza huu mpango manake ilibidi nikubali kwamba kama kuimba nimeshaimbwa, kwa sababu kutakua na pande mbili za hiyo movie, itauzwa kama movie ya kawaida, na pia itauzwa kopi ya behind the scene"by japhet

MPIGIE KURA GODZILLA TUZO ZA KILI TANZANIA MUSIC AWARDS

Mpigie kura Godzilla. Kili Tanzaia Music Awards " Msanii bora wa hip hop"  andika P1
wimbo bora wa hiphop  " King Zilla" feat Macochali, andika Z2, kwenda number 15747.

KANYE WEST ASEPA NA TUZO YA GRAMMY "BEST RAP ALBUM"

Kanye West ameondoka na ushindi mkubwa katika upande wa hiphop, jana katika tuzo za 54 za Grammy. kanye alienda home na tuzo ya Rap Album Of The Year kwa My Beautiful Dark Twisted Fantasy album.
Kanye pia ameondoka tuzo ya Best Rap Collaboration kwa “All Of The Lights” akiwa na Rihanna, Fergie, Elly Jackson and Elton John.
collaboration yake pia  “Otis” na Jay-Z and Otis Redding pia imechukua Best Rap Performance.
Jay Z na kanye kwa pamoja licha ya kutoa bonge moja la album "Watch the throne" wameskip the Grammy awards.
washindi wengine ni pamoja na Chris Brown, ambae ameshinda tuzo ya best R&B album kwa F*A*M*E na Cee Lo Green, ambae alishinda Traditional R&B Vocal Performance na Best R&B Song kwa “Fool For You” na Hallim & Jack Splash.
Adele pia ameondoka nyumbani na tuzo 7 za grammy kwa album yake inayoitwa album 21 na hit single “Rolling In The Deep,”by japhet