Wednesday, July 17, 2013

MTAZAME DUDE WA BONGO DAR ES SALAAM ALIVYOIGIZA KWENYE MUSIC VIDEO YA YAHAYA YA LADY JAY DEE KOMANDO.










bonge la video itakuwa

angalia picha za thiago akikabiziwa jezi na cavani asaini rasmi PSG






EXCLUSIVE: HUMUD - "LONGOLONGO ZA AZAM ZINANIFANYA NIKOSE NAFASI YA KWENDA KUCHEZA JOMO COSMOS YA SOUTH AFRICA'


Miezi mitatu baada ya kuripotiwa kufuzu majaribio ya kucheza soka la kulipwa katika timu ya Jomo Cosmos FC ya Daraja la Kwanza nchini Afrika Kusini, ndoto za kiungo wa kimataifa wa Tanzania na Azam FC Abdulhalim Humud kucheza kwenye klabu hiyo inayoshiriki kwenye ligi kuu ya Afrika ya kusini zimeanza kufifia baada ya kushindwa kujiunga na timu hiyo baada ya taratibu za usajili wake kukwamisha na Azam FC.


Kwa mujibu wa Humud ambaye amewahi kuvitumikia vilabu vya Mtibwa Sugar ya Morogoro na Simba, anasema yeye binafsi alikamisha kila kitu katika kuhakikisha dili lake la kwenda Cosmo linafanikiwa na hata alishakubaliana maslahi binafsi na timu hiyo inayomilikiwa na kufundishwa mwanasoka wa zamani wa nchi hiyo 
Jomo Sono.

"Mie nilikamilisha majaribio yangu na nikafuzu na siku tano kabla sijaondoka kule tayari nilishakubaliana kila kitu na klabu ya Jomo Cosmos. Niliporudi huku nyumbani Azam wakaniambia kila kitu kitakuwa sawa, pia walinipa barua ya kunijulisha kwamba sitokuwepo kwenye usajili wa Azam FC msimu ujao kwa kuwa nitauzwa kwenda Jomo.

"Niliwaachia Azam kila kitu katika kukamilisha taratibu za usajili kwa sababu ndio walikuwa wanasimamia hivyo vitu, lakini mpaka jana siku ya mwisho kukamilisha usajili hakukuwa na lolote lilofanyika. Tarehe ya mwanzo ya kukamilisha usajili na kwenda South ilipita ikabidi niende ofisini kuulizia na wakaniambia kila kitu kinaenda sawa na jana tarehe 15 ilikuwa ndio niondoke, lakini bado kimya.

"Kiukweli hili linakatisha tamaa, ukizingatia hata nauli ya kwenda kwenye majaribio nilijitolea mwenyewe, sio klabu wala mtu yoyote ambaye alinitolea, ilinitoka dola 800 kutoka kwenye mshahara wangu. Kiukweli napata machungu sana kuhusu suala hili. Muda mwingine tunaonekana wachezaji ndio tuna matatizo lakini ni hawa viongozi wa vilabu.,' alisema Humud

Aidha katika barua rasmi aliyoandikiwa na Azam FC kuhusu uhamisho wake wa kwenda Jomo Cosmos, (mtandao huu unayo nakala) klabu ilimthibitishia Humud kwamba ameuzwa kwenda Jomo na kutokana na hilo imemuondoa kwenye usajili wa msimu ujao, lakini pia endapo tu ingeshindikana kukamilika kwa usajili wake basi angerudi Azam FC. Hata hivyo kwa sasa tayari Azam imeshamtema mchezaji huyo na pia uhamisho wake wa kwenda Jomo unaelekea kushindikana na kumuacha mchezaji huyo asijue nini atafanya msimu ujao wa ligi.

Tetesi za chini kutoka vyanzo vilivyo karibu na klabu ya Azam ni kwamba - Humud alikuwa hapatani na kocha Stewart Hall na hivyo alikuwa akitafutiwa namna ya kuondolewa kwenye timu hiyo.duh kwel Tanzania tutafika.

Chris Brown adai kufuta Graffiti zake kwa upendo wake mwenyewe na si kwa kulazimishwa na Jiji

Chriss brown leo hii ameoneka akitemana na graffiti yake aliyokuwa ameichora kwenye ukuta wa mbele wa nyumba yake iliyoko Hollywood, baada ya kutakiwa kufanya hivyo, na jiji la LA  baada ya majirani kulalamika kuwa hazileti picha nzuri na zinatisha watoto wao.
Ripoti za mwanzo zilikuwa zinadai kuwa CB alikuwa anapingana na jiji la LA  tangu mwezi May kuhusu graffiti hiyo iliyokuwa imechorwa jitu la kutisha (monster), na kupinga kuifuta kwa kudai  kuwa inalindwa na  1st Amendment ya mwaka 1792 inayodai serikali kuheshim mawazo ya aina hiyo
 lakini baada ya kushindwa kwa vita hiyo Brown amesema, ameamua kufuta kwa upendo wake yeye mwenyewe na si kwa kalazimishwa na jiji hilo au kwa  kutishiwa kulipishwa fine kubwa kw akosa hilo
Baada ya majirani kulalamika kuhusu picha hizo, jiji lilimtisha kwa kumpiga fine kubwa kama hataifuta ----leo hii wameonekana wafanyakazi wakipaka rangi nyingine juu ya michoro hiyo.
kwa vyovyote vile, idara ya ujenzi kitengo cha  usalama cha  LA imesema kama wakaguzi wao wataridhika na ufutwaji wa graffiti hiyo, basi CB hatapigwa fine hiyo siku ya kesho.aliyafuta kabla ya fine

 

Baada ya wanajeshi wa 7 wa Tanzania kuuwawa: Tanzania yapendekeza UN kufanyia marekebisho sheria ya kulinda amani

Baada ya walinda amani saba wa Tanzania kuuawa na watu waliokuwa wamejihami eneo la Darfur mwishoni wa wiki, na wengine wengi kujeruhiwa na baadhi wakiwa mahututi, Tanzania imependekeza kufanyiwa marekebisho sheria ya kulinda amani ya UN, ili kujikinga na mashambulizi.

Mauaji ya walinda amani 7 wa Tanzania nchini Sudan yamewashangaza wengi sana nchini humo kulingana na naibu waziri mkuu, kwani nchi hiyo ndio imeanza kushika kasi katika juhudi zake za amani kimataifa. . 
Maafisa hawakuwa na taarifa kamili kuhusu uvamizi wa Jumamosi ambapo wanajeshiu wengine 17 walijeruhiwa vibaya katika shambulizi baya zaidi kushuhudiwa dhidi ya vikosi vya kimataifa nchini Sudan
.
Shambulizi hilo lililofanywa na kikundi kikubwa cha watu waliokuwa wamejihami, ilihusisha mashambulizi makali ya mizinga na iliyolenga wanajeshi hao umbali wa kilomita 25 Magharibi mwa mji wa Khor Abeche.

Tanzania, ambayo pakubwa ni nchi salama na thabiti katika Kanda ya Afrika Mashariki, imeendelea kujitolea sana katika juhudi za amani duniani.
Mwaka jana ilikuwa nchi ya kwanza kujitolea kupeleka vikosi vyake Mashariki mwa Congo, chini ya kile ambacho kitakuwa kikosi cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa wenye jukumu la kupambana vilivyo na makundi ya waasi huko.

Thursday, July 4, 2013

NEW SONG YA CHRIS BROWN FT AALIYAH

cpwaa asaini mkataba mnono



Cpwaa amesaini mkataba na  moja ya lebo kubwa kabisa za muziki duniani “Universal Music, South Africa”.Maudhui yake yatasambazwa kupititia Kleek ( mobile streaming service) inayopatikana kwenye simu zote za Samsung (Smart phones) katika nchi za  Ghana, Angola, Kenya, South Africa na Nigeria.

 CPwaa ni mmoja kati ya wasanii namba moja waliosainiwa na Universal Music kutoka East Africa kwa ajili ya Kleek continental platform.

 March 13, 2013 Universal Music Group, wakishirikiana na Samsung pamoja na lebo za Africa na za kimataifa, wamezindua pan-African mobile music streaming service inayoitwa Kleek, iliyodizainiwa na kutengenezwa kwa ajili ya Africa .

 Kleek itawaweka karibu wapenzi wa muziki na wasanii wao wanaowapenda, huku ikiwapatia nafasi muhimu kwa wasanii kuwa na access na watu wengi
Licha ya kupata mapato kupitia mziki wake, Cpwaa pia atapata nafasi ya kujulikana duniani na ulimwenguni kote kupitia Kleek.