Friday, December 20, 2013

EXCLUSIVE:Balozi Kagasheki atangaza kujiuzulu




kagasheki
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Balozi Khamisi Kagasheki ametangaza nia ya kujiuzulu wadhifa wake dakika chache zilizopita bungeni  mjini Dodoma,sababu kubwa ya kujiuzulu ni baada ya kusomwa  ripoti ya kamati ya Bunge Kumtuhumu kuzembea na kukithiri kwa vitendo viovu vilivyofanywa na wanausalama wakati wa Operesheni Tokomeza.
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira imebainisha kuwa oparesheni Tokomeza Ujangili iliyoendeshwa na Serikali ilikumbwa na unyanyasaji mkubwa wa wananchi, Ukatili, Udharirishaji, Ubakaji na Mauaji huku baadhi ya wazazi wakivuliwa nguo, kuteswa na kubakwa mbele ya wanafamilia.
Akiwasilisha bungeni taarifa ya kamati hiyo Mwenyekiti wake James Lembeli amesema pamoja na mateso hayo yaliyowakumba wananchi pia nyumba zao zilichomwa na mifugo kupigwa risasi huku mingine ikifa kwa kukosa maji, chakula na maziwa kwa ndama wadogo.
Kamati hiyo pia imebainisha kuwepo kwa vitendo vya Rushwa vilivyotawala oparesheni Tokomeza ambapo pia wananchi waliokuwa na mifugo walitozwa faini na mifugo mingine kuuzwa kwa bei nafuu ambayo haikulingana na faini iliyokuwa ikitoza na wafugaji walizuiwa kushiriki mnada wa uuzaji wa mifugo hiyo.

Friday, December 6, 2013

EXCLUSIVE:Makundi ya kombe la dunia 2014 yametangazwa, ndio haya.

fifa 1
June – July 2014 ndio fainali za kombe la dunia huko Brazil ambapo makundi yameshapangwa tayari, cheki mzigo wenyewe ulivyopangwa…
Group 1
group 2
group 3
group 4
group 5
group 6
group 7
group 8

ujio mwengine wa shetta;Shetta amshirikisha Diamond Platinumz kwenye wimbo wake mpya 'Mama Qayllah' soon utakuwa hewani



 Ile collabo iliyofanya vizuri mwaka 2012  kati ya Shetta na Diamond Platinumz inajirudia tena mwishoni mwa mwaka huu,ambapo wasanii hao wawili wameamua kuingia studio na kutengeneza wimbo mpya unaoitwa kwa jina la Mama Qayllah.

Shettta amesema kuwa tayari ameshafanya ngoma hiyo mpya na Diamond Platinumz inayoitwa Mama Qayllah ambayo imetayarishwa na Shedy Clever wa Burn Records.

'Napenda kutoka shukrani za dhati kwa mashabiki wa muziki wa Bongo Fleva kwa kunielewa kwa kile ninachokifanya katika tasnia ya muziki pia ningependa kuwaambia  kwamba ninatarajia kuachia wimbo mpya hivi karibuni ambao nimefanya na Diamond,ngoma inaitwa 'Mama Qayllah' producer aliyesimamia Vocal,Mixing ni Sheddy Clever wa Burn Records,kwa hiyo mashabiki  wakae mkao wa kula, hapa Shetta ama Baba Qayllah pale Diamond wa Wasafi Classic Baby,aahaha hatari'Alisema Shetta.

Kaa Tayari kwa ujio huo mpya kutoka kwa Shetta ft Diamond 'Mama Qayllah'

Thursday, December 5, 2013

Nelson Mandela aaga dunia

 
Rais wa zamani wa Afrika Kusini ameaga dunia . Habari zaidi zitakujia hivi punde