Thursday, July 19, 2012

STAA BONGO MOVE APIGWA STOP KUIGIZA

Posted by japhet
Nyota  kutoka tasnia ya  filamu Bongo Skyner Ally huenda asionekane tena kwenye ulimwengu wa move kufuatia kupigwa  stop kushiriki katika  kuigiza.
Stori  'under carpet' ambazo Teentz.com imezinyaka kutoka kwa mmoja wa wapambe wa mwigizaji huyo aliyeng'arisha nyota yake kupitia filamu ya  'SECOND WIFE' iliyopikwa na mkali Ray Kigosi, zinasomeka kuwa  Skyner amepigwa stop na  wazazi wa  upande pili  (wakwe) ili aweze kulea vizuri mtoto wake badala ya kutumia muda mwingi akiwa kambini na waigizaji wengine kwa ajiri ya kurekodi 'muvi'.
"amezuiwa, na sijui kama ataruhusiwa kipindi cha  karibuni  na  huenda  ikawa moja kwa moja  kwani ameambiwa atulie alee familia na mtoto wake, alisema mpambo huyo.…

IMAGES FROM #LEKADUTIGITE KIGOMA ALL STARS CONCERT IN KIGOMA...!!!

All musicians and MPs on stage.
MPs on stage.
Diamond Platnumz on stage.

Boys making the most of it.
Crowd.
Halima Mdee and Esther Bulaya.
Zitto Kabwe welcomes other Mps.
...Woman with purple umbrella following the show.
...The show continues.

TIWA SAVAGE, WIZKID, MABALOZI WAPYA WA PEPSI KUTOKA NAIGERIA

baada ya miezi kadhaa ya maneno ya chini chini, sasa imethibitishwa kuwa wawili hawa ndio mabalozi wapya wa PEPSI. Tiwa Savage na Wizkid walitangazwa usiku wa jana katika exclusive event iliyofanyika Likwid ndani ya Lagos

P SQUARE WAMPOTEZA MAMA YAO

Wasanii wakubwa nchini Nigeria na duniani kote, P-Square wamempoteza mama yao mzazi Mrs Okoye usiku wa kuamkia leo nchini India alipokuwa amepelekwa kwa matibabu baada ya kuhamishwa kutoka katika moja ya hospitali kubwa nchini Nigeria, St Nicholas iliyopo Yaba, Lagos.
inasemekana mama wa wasanii hao, alikua ni moja kati ya nguzo yao kubwa kimuziki kwa kuwapa ushauri na upendo usio na gharama yoyote.
arrangement zinafanyika ili kuurudisha mwili wa marehemu nchini Nigeria.

MATUKIO YA UOKOAJI WA WATU WALIOZAMANA NA MELI YA MELI YA STAR GATE HUKO KATIKA BAHARI YA CHUMBE ZANZIBAR

 Meli ya Mv Skagit iliyokuwa safarini kutoka Dar kuelekea Zanzibar imezama majira ya saa nane mchane hivi leo katika maeneo Pungume na Chumbe baada ya kukumbwa na upepo mkali.

Meli hiyo inayosadikiwa kuwa na abiria 250 inasemekana imepindukia upande mmoja na huku abiria wengi wakiweza kuokolewa kutokana na jitihada mbali mbali kupitia vile vile msaada wa boti za Mv Kilimanjaro, Tug ya Bandari na vyombo vyengine.

Mpaka tunandika taarifa hizi ni maiti tatu zilikwishapatikana na kiasi cha abiria 150 wameokolewa na waliojeruhiwa wanatibiwa katika Hospitali ya Mnazimmoja. Taarifa zinaeleza kwamba kulikuwa na watoto takriban 30 na Watalii kutoka nchi mbali mbali wafikao kumi.

Wazamiaji kutoka Kikosi cha KMKM pamoja na Jeshi tayari wapo eneo la ajali kusaidia kuokoa maisha ya wananchi waliokumbwa na maafa haya. 
 Majeruhi alieokolewa katika meli ya Star Gate iliozama huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250. Picha/Ramadhan Othman Ikulu
.
Inawezekana taarifa za ajali ya boti ya Seagul iliyotokea leo (July 18) mchana Zanzibar ukawa umezisikia au kuzisoma sehemu mbalimbali lakini kauli hii ya Waziri wa mambo ya ndani imetoka kwenye taarifa ya habari ya saa mbili usiku. 
Waziri Emmanuel Nchimbi akiongea kwenye taarifa ya habari ya saa mbili usiku july 18 2012  TBC1 alisema “vikosi vya uokoaji vinaongozwa na mkuu wa jeshi la polisi Inspekta Jenerali Said Mwema vinaendelea na uokoaji”
Kuhusu watu waliopoteza maisha au kuokolewa Waziri Nchimbi amesema “Katika abiria wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 250 waliokua wamebebwa na boti hiyo, wameokolewa 124 wakiwa hai na waliothibitishwa na jeshi la polisi kufariki dunia ni saba tu, juhudi kubwa za uokoaji zinaendelea”
.