MAAFANDE WAHUSISHWA NA TUKIO LA UTEKAJI WA MWENYEKITI WA JUKWAA LA WAHARIRI, ABSALOM KIBANDA
HII NI KAULI YA ABSALOM KIBANDA BAADA YA KUTEKWA...............
"Baada
ya kutoka kwenye gari, nahisi nilikanyaga sehemu mbaya, nikateleza na
kuanguka wakanifuata...niliona kama watu watatu hivi wakaanza
kunishambulia. Sikuwa nafahamu kilichojiri, lakini nilisikia mwingine
akimwambia mwenzake afande 'mshuti... mshuti' huyo alipoelekeza mtutu na
kujaribu 'kushuti' (kupiga risasi) ilikuwa kama vile imegoma.
“Nikiwa bado niko chini, wakanipiga kwa kitu cha ncha kali kwenye jicho
la kushoto, wakaning’oa meno na kucha katika vidole vya mkono wa kulia,
walinipiga sana na nilipata maumivu makali. Baada ya kunipiga na
kunijeruhi waliniburuza hadi bembeni ya nyumba yangu na kunitupa na
wakaondoka, baadaye majirani na wasamaria wema walikuja kuniokoa..."
No comments:
Post a Comment