Friday, August 16, 2013

NGASA APIGWA RUNGU NA KAMATI YA SHERIA

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imepitia usajili wa wachezaji wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom na kumuidhinisha Mrisho Ngasa kuchezea timu ya Yanga baada ya kukamilisha usajili wake.
Hata hivyo, Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa imebaini kuwa Ngasa alisaini mkataba mwingine Simba (katika kipindi ambacho alikuwa na mkataba na Azam) ambapo anatakiwa kurejesha fedha alizopokea (sh. milioni 30) pamoja na fidia ya asilimia 50 (sh. milioni 15) ya fedha hizo kwa Simba.
Kamati pia imemfungia mechi sita za mashindano (kuanzia mechi ya Ngao ya Jamii), na anatakiwa awe amelipa fedha hizo ndani ya kipindi hicho cha kukosa mechi hizo. Akishindwa, hataruhusiwa kucheza hadi atakapolipa fedha hizo.
Vilevile Kamati imepitia pingamizi zote zilizowasilishwa kuhusu usajili wa wachezaji, kukatiza mikataba ya wachezaji na kuzitaka klabu husika ziwe zimetatua masuala hayo hadi Alhamisi (Agosti 22 mwaka huu).
Kwa upande wa wachezaji wa kigeni, Kamati imeagiza wasiruhusiwe kucheza hadi watakapopata Hati za Uhamisho wa Kimataifa (ITC) pamoja na vibali vya kufanya kazi nchini (work permits).
Kamati hiyo itakutana tena Ijumaa (Agosti 23 mwaka huu) ili kupata ripoti za pingamizi ilizoagiza ziwe zimefanyiwa kazi hadi Agosti 22 mwaka huu na kutoa uamuzi kwa pande ambazo hazikuafikiana.

Hatimaye Muigizaji Elizabeth Michael (Lulu) arejea kazini, anazindua movie yake ya kwanza tangu kutoka jela tarehe 30 August


Muigizaji Elizabeth Michael (LULU) anatarajia kuachia movie yake ya kwanza tangu alipotoka jela "Foolsh Age" siku ya tarehe 30 mwezi wa nane katika ukumbi wa Mlimani City huku kukiwa na wasanii wa muzini pamoja na Jay Dee na Machozi Band ambao watasindikiza uzinduzi huo.

hotlulumichaelNina kila sababu ya kumshukuru Mungu....!!!ninafuraha ya kuwafahamisha kuwa TAREHE 30/8/2013 ndio siku nitakayozindua movie ya mpya ya FOOLISH AGE....hatimaye narudi kazini!!!!Uzinduzi utafanyika katika ukimbi wa MLIMANI CITY....kutakuwepo na wasanii mbalimbali wa muziki....na pia LADY JAY DEE pamoja na MACHOZI BAND atakuwepo pia!!!nahitaji support ya mashabiki wote wa LULU na mashabiki wa BONGO MOVIE.....♥♥♥♥!!!#PROINPROMOTERS

Thursday, August 15, 2013

Video: Lakuchumpa Joti na Godzilla


Baada ya muda mrefu kupita tangu collable ya mchekeshaji "Joti" na rapper Godzilla kudondosha bonge la hit "Lakuchumpa" sasa wamedondosha video ya wimbo huo..

Diddy amkejeli Kendrick Lamar. nouumaaaaaaaa saaaaaaaaaanaaaaaaaaaa

Mashambulizi dhidi ya Kendrick Lamar yazidi kuongezeka, hasa pale Diddy alipomuwashia moto kupitia Instagram, nakuthubutu kumuingiza Jay Z kwenye mashambulizi hayo.
Lamar amejikuta katika mashambulizi kutoka kwa Rappers mbali mbali ndani ya masaa 34 baada ya kuvuja kwa ngoma ya Big Sean "Control" ambapo ndani yake kuna mistari yake iliyokuwa ikiwaponda ma-rapper hao na kudai kuwa yeye ni King wa New York.
Diddy ameamua kumshambulia kwa kutumia picha yake akiwa na Jay Z (Mabosi wengine wa NY) wakicheka huku akiambatanisha na maneno yanayomkejeli Kendrick Lamar
"Nakisha Kendrick akasema "mimi ni King wa NewYork"
Diddy sio wa kwanza kumrudishia mashambuliz Lamar, NBA Legend mwenye miaka 67 Phil Jackson aliachia maneno kupitia ukurasa wake wa twitter baada ya Lamar kumtaja kwenye mashairi hayo

godzila ft joti -lakuchumpa bonge la video

duhhhhhhhhhhhhhhh nouma saananananananananana

Wednesday, August 14, 2013

Baada ya mashabiki kurusha makopo stejini kisa Diamond kuchelewa kupanda hizi ndio sababu zinazosemekana za kushelewa kwake kupanda.......


Baada ya umati wa watu waliohudhuria show ya Platnum wakirusha makopo stejini baada ya Diamond kuchelewa kupanda hizi ndio sababu zilitajwa kupelekea kuchelewa kwake.
mtandao wa kenya Ghafla umeripoti kuwa Diamond alichelewa kwasababu alikua akijifanya "Diva" pale ambapo kwa maksudi alijichelewesha Tanzania na hivyo kuchelewa ndege kuelekea Kenya.
Baada ya kuchelewa ndege Diamond alidai aletewe ndege binafsi (Private Jet) na National Media Group (NMG) ambapo iliwabidi wafanye hivyo.
So you wonder what led to Diamond being delayed?Apparently the concert was delayed because the 'Nataka Kulewa' singer was being a total diva.It is said that Diamond deliberately stalled in Tanzania  therefore missing his plane to Kenya, he then demanded a private jet from the Nation Media Group. NMG had to bend over backwards  and charter a  private jet for the Tanzanian Superstar.
Mda mfupi baada ya Diamond kutua Mombasa aligoma ku-check in katika hoteli aliyoandaliwa (Mombasa Beach Hotel)  ambapo ndipo show ilipokuwa ikifanyika na kusisitiza kuchukuliwa presidential  suite White Sands Hotel ambayo iliwagharim mkwanja mrefu NMG.
Baada ya mahitaji yake kukamilishwa ndio Diamond alikubali kupanda stage, ila baada ya kukitifua mbaya stejini  kama wa kweli kwa show na perfomance ya hatari na kuwaacha watu wakiwa na historia isiyofutika leo wala kesho, show ambayoinayoweza kuelezeka kama ya ki legendary.Mashabiki walitulia na kuimba nyimbo zake mwanzo mwisho..
mtangazaji katika video hii badala ya kusema Nasibu Abdul yeye kasema Kassim lol

Friday, August 2, 2013

BRAND NEW : OMMY DIMPOZ FT J MARTIN "TUPOGO"

Ni ngoma mpya ya Omary Nyembo aka Ommy Dimpoz inayokwenda kwa jina la 'TUPOGO' akiwa amemshirikisha J Martin

Bonyeza hii link uweze kuisikiliza http://beta.hulkshare.com/ixjduj028pog

Bow Wow am-kiss tena Tyra Banks, safari hii kwenye kipindi chake 106&Park ebwana duhhhhhhhhhhhh


Ikiwa ni miaka 4 (2009) tangu Bow wow alipom-kiss Super Model Tyra Banks kwenye kipindi chake mwenyewe mwanadada (The Tyra Banks Show), Bow wow amerudia tena kitendo hicho na safari hii ikiwa ni kwenye kipindi anachokiendesha Bow wow (106&Park), ambapo jana Tyra alikuwa ni mgeni rasmi katika kipindi hicho.
Bow Wizzy alipopata chance tu, alijisogeza karibu na Tyra pia alisogea na kuweka mapaja yake juu ya mapaja ya Bow wow na Tayra akatupia lips zake kwenye lips za dogo na Bow wow kuonekana kuridhiiiika hatari, huku akiendelea kujisifia yeye ndio mtangazaji bora zaidi wa kiume kwenye upande wa TV