Msanii wa kizazi kipya Naseeb Abdul aka Diamond Platinum jana alizindua
video ya wimbo wake mpya 'Number One' kwenye hoteli ya kifahari 'Serena
Hotel' iliyopo jijini Dar es Salaam.
Katika uzinduzi huo pia Diamond alimpa zawadi ya gari Msanii Mkongwe Ngurumo aliyetangaza kustaafu siku za hivi karibuni.
Diamond alisema amesikitishwa sana baada ya kusikia msanii huyo kustaafu
katika muziki na bila kumiliki gari lolote katika enzi za ujana wake
mpaka uzeeni ndio sababu ya kumpa zawadi ya gari aina ya Funcargo.
No comments:
Post a Comment