EXCLUSIVE:DOGO JANJA HAYUPO TENA MTANASHATI
Janjaro
msanii kutoka Arusha lakini makazi yake yapo Dar amefunguka kuwa hajafukuza na Ostaz Juma Namusoma kwenye kampuni yake
ya Mtanashati bali amejitoa mwenyewe kwa hiari yake. Janjaro amesema
amechoka na matendo tu ya Ostaz na alikuwa tu akiyavumilia lakini kwa
sasa ameshakuwa mkubwa so nataka nikae kivyangu vyangu nifanye mambo
yangu kama wasanii wengine ambao hawana meneja na wanafanya poa.
Namnukuu Janjaro akisema....
"Najua yatasemwa mengi
kutoka kwa Ostaz Juma ila mimi ndio uwamuzi wangu, kuna watu wanasema
sina utovu wa nidhamu lakini hao watakuwa wananijua sasa hivi
hawajanifuatilia kutoka nyuma. Hata mtoto mdogo atakuwa mtundu ila akiwa
mkubwa hunyooka na kuwa mtoto mzuri sasa nimekuwa mkubwa na kupelekwa
pelekwa tena sitaki, kwa maelezo zaidi Ostaz Juma aongee na wazazi wangu
asiongee na mimi"
No comments:
Post a Comment