Friday, September 27, 2013

Huu ndio ujio mpya wa C-Pwaa.nouma sanaaaa

Mashabiki wake hupendelea kumuita "King of BongoCrunk"....jina halisi ni Ilunga Khalifa a.k.a CPwaa! Msanii wa muziki wa kizazi kipya Tanzania ambaye baada ya ukimya mrefu sasa kuachia kazi zake mpya.
C.P a.k.a CPwaa mwenye tuzo 3 za Tanzania Kilimanjaro Music Awards na Multiple Channel O Africa Music Video Awards nominations anakuja kivingine kabisa mwaka huu. Tarehe 1 mwezi wa October 2013, CPwaa ataachia single yake mpya na ya kwanza kabisa kwa mwaka huu.Single hiyo iitwayo "Chereko Chereko" yenye mahadhi ya AfroDance imefanywa chini ya studio za 'De Fatality Music" na producer "Mesen Selekta" ambaye mwaka huu alichukua tuzo ya mtayarishaji  bora Tanzania anayechipukia.Nyimbo hii itapatikana kwenye mitandao yote na media zote kuanzia tarehe moja October.
CPwaa ambaye amesaini mkataba mnono na Universal Music group vile vile anategemea kuachia single nyingine mwanzoni mwa mwaka 2014 ambapo amewashirikisha mafahari wengine wawili kutoka Afrika. Single hiyo ya kimataifa iitwayo "Cross-Borders Therapy" imekutanisha wakali kutoka mashariki,magharibi na kusini mwa Afrika. CPwaa amemshirikisha "DBlack" kutoka Ghana, DBlack ni moja ya wasanii wakubwa wa Hip Hop Afrika ambaye ana tuzo nyingi ikiwemo zile za Channel O.Kwa upande wa Afrika ya kusini CPwaa amemshirikisha "Hip Hop Pantsula" a.k.a HHP kwenye nyimbo hiyo hiyo ya Cross Borders Therapy.HHP ni mmoja ya MaMC wakali kutoka bondeni mwenye tuzo nyingi ikiwemo ya MTV Base. Nyimbo hii itakuwa ya kwanza Afrika ambayo imekutanisha wakali kutoka mashariki ,magharibi na kusini ( The first East,West and South African Hip Hop Collaboration in History).Nyimbo hii pia imefanyika chini ya producer Mesen Selekta pale  "De Fatality Music" Studio.
Kifuatacho baada ya nyimbo hizi kutoka ni video zake ambapo Chereko Chereko itafanyiwa Tanzania na Cross Border Therapy kufanyika nchini Afrika ya kusini. Kwa wale mashabiki ambao watakuwa na kiu ya wimbo wa Cross Border Therapy ambao utatoka mwakani wataweza kuupata wimbo huo kupitia iTunes,Amazon, Spotify na digital store zingine bila kusahau mtandao wa "The Kleek" kwa wale watumiaji wa smartphones za Samsung na Androids.

Wednesday, September 25, 2013

Hii ndiyo list ya wasanii 10 wa Hiphop waliongiza pesa nyingi kwa mwaka 2012/13, mjue na mwanamke mmoja ambaye yupo kwenye list hii.duh noooma sana


0x600Forbes.com wametoa list wasanii wa Hiphop ambao wameingiza pesa nyingi sana kwa muda wa miezi 12 iliyopita.  List imeanza na msanii tajiri kuliko wote kwenye muziki wa Hiphop na kuna mwanamke mmoja tu ambaye yupo kwenye hii list.

1. P. Diddy
Forbes wameandika kwamba Diddy ameingiza zaidi ya dola millioni 50 kwa muda wa miezi 12 iliyopita. Vyanzo vyake vikubwa ni  Ciroc Vodka,Sean  John,Bad Boys, Blue Flame agency pamoja na mkataba wake mpya na Warner Cable kwa ajili ya Revolt TV
2. Jay Z
Jay Z ameingiza dola millioni 43, vyanzo vyake vikubwa ni Armand de Brignac champagne, D’Ussé cognac, Roc Nation label/management firm. Pia album yake ya Magna Carta Holy Grail ambayo Samsung waliweka investment ya dola millioni 5. Pia Jay anabiashara nyingine kama uwakala wa wanamichezo mashuri kama Kelvin Durant na pia aliuza share zake za Brooklyn Nets.
3. Dr Dre
Ameingiza dola millioni 40.Kama kawaida ya Dr Dre, pesa nyingi anavuta kutokana na headphones na earphones za Beats by dre. Pia anafanya upanuzi wa kampuni zake nyingine
4.Nicki Minaj
Ame-gross dola millioni 29, mwanamke pekee kwenye list amepata pesa hizi kwenye show nyingi anazofanya, mkataba wake wa Ameican Idol,mikataba yake na vinywaji kama Pepsi.
5.Birdman
Pesa alizongiza ni dola millioni 21, record label yake inawasanii wakubwa kama Lil Wayne,Drake na wengine. Pia vyanzo vingine ni kama nguo za YMCMB,Vodka na publishing.
6.Kanye West
Mkali wa Yeezus ameinginza dola millioni 20, album yake mpya ni moja ya vyanzo vikubwa sana kwake. Pia Kanye anamikataba,show nyingini na clothing line ya Donda West.
7.Lil Wayne,
Lil Wayne ameingiza dola millioni 16, show,Young Money na nguo za Trukfit ni vyanzo vikubwa kwake
8.Wiz Khalifa
Dola millioni 14 zimeingia kwenye account yake, show zaidi ya 75 baada ya nyimbo zake kufanya vizuri ndiyo vyanzo vikubwa vya pesa zake.
9.Ludacris
Mkali wa fiesta ameingiza dola millioni 12, vyanzo ni headphones za Soul by Ludacris,show zake na role yake kwenye movie ya FF6.
10.Pitbull
Fungu lake ni dola millioni 11 ambapo zinatokana na album yake ya Global Warming, tours  na endorsements na Kodak pamoja na Dr. Pepper.

Friday, September 20, 2013

Ommy Dimpoz akiwa ndani ya VOA (Voice Of America) akihojiwa kuhusu mziki wake

Ommy Dimpoz ambae  yuko Marekani kwa ajili ya shows kadhaa ndani ya wiki 3 zilizompeleka huko, amepata nafasi ya kuhojiwa na kituo cha VOA, na kuzungumza mengi juu ya muziki wake.

Dimpoz akihojiwa na mtangazaji wa kituo hicho "Sunday Shomari" ambapo alizungumzia kuhusu matatizo ya wasanii kutumia madawa ya kulevya nchini, historia yake katika kazi yake ya muziki, tour iliyompeleka huko, malengo yake ya baadae na mengine mengi.
Dimpoz anatarajia kuanza show yake ya kwanza ndani ya Washington DC siku ya kesho na tayari mpaka sasa meza za VIP zimeshauzwa zote na kiingilio chake ni dola 30 kwa wale wa kawaida kweli mziki wetu unakuwa juu.

Dogo Janja kushoot video ya "serebuka" Arusha .nouma sana

Dogo Janja chini ya mtanashati, anatarajia ku-shoot video ya wimbo wake mpya "Serebuka" jijini Arusha.

"Nashootia Arusha na video itakuwa ya utofauti, itaonyesha uhalisia wa miziki ya uswahilini na watu wanavyo serebuka kingaleloo, naamini video yanguitakuwa simple halafu kali. Nawaza kufanya na Dx au Nisher maana ndio naanza connection nao, nikipata jibu la uhakika nitawaambia mashabiki wangu" amesema Janjaro.

mcheck BANDANA akifanya yake kwenye shindano la SM na kesho ndio fainal yan nouuma sana check chini

Thursday, September 19, 2013

Shetta akikaguliwa begi lake kama mtu asiye aminiwa Airport Zanzibar nouuuuma sanaaaaaaaa

Msanii Shetta ameonekana kukerwa na kitendo cha kukaguliwa begi lake  na kutoa kila kitu kilichokuwa ndani ya begi lake kwa ajili ya kukamilisha ukaguzi huo, katika uwanja wa ndege wa Zanzibar akisafiri kuelekea Mombasa akiwa na msanii mwenzake kutoka kiumeni "Chege"



Kutokana na matukio ya watanzania wengi kujihusisha na usafirishaji wa madawa haramu ya kulevya, serikali imekuwa makini sana kwa wasafiri wanaotumia usafiri wa anga kutoka na kuingia ndani ya nchi, kuhakikisha hakuna kila anaejihusisha na kazi hiyo kufikishwa katika mikono ya sheria.

Wednesday, September 18, 2013

sikiliza mistari ya mbagala kwenye lugha ya kingereza nouma sana

Hiki ndicho alichokiandika Criss juu ya kuimba wimbo huu

As a language exercise, I picked a Swahili pop song that I like and attempted to transcribe the lyrics and learn to sing it. The Swahili lyrics are below as well as my attempted English translation. Mbagala is an impoverished district on the outskirts of the Tanzanian city Dar Es Salaam. I might have made some mistakes in the transcription or translation, so kama wewe ni Mswahili na unalo shauri lolote kuhusu maneno au tafsiri, niambie!


Mbagala by Diamond

Verse 1

Busara na upole
(Wisdom and kindness)
Na hekima niliyorithi kutoka kwa mama yangu, mama
(And knowledge which I inherited from my mother)
Vyote hukuvijali, ukaona silingani kabisa kuwa na wewe
(You didn't care about any of it, you saw that I'm too different to have you)
Kwa kuti na mkole, ukakata kabisa na shina la penzi langu na
(For the palm frond and tree, you completely cut the stem of my love)
Eti kisa mali, ukaona bora uniache mimi na uolewe
(Oh, because of money, you thought it good to leave me and get married)
Ile siku shehe namuona anachoma ubani
(That day I see the sheikh burning incense)
Unavishwa pete unakuwa mke wa fulani
(You are wearing a ring and are becoming someone's wife)
Niliumia sana, sana
(I was hurt badly)
Ile siku shehe namuona anachoma ubani
(That day I see the sheikh burning incense)
Unavishwa pete unakuwa mke wa fulani
(You are wearing a ring and are becoming someone's wife)
Niliumia sana, niliumia sana, sana
(I was hurt badly, I was hurt so badly)

Chorus

Tatizo kwetu Mbagala, hapa nyumba mbele jalala
(The trouble in Mbagala, at the house here in front of the dump)
Tatizo kwetu Mbagala, ukaona mapenzi siwezi
(The trouble in Mbagala, you saw I cannot love)

Verse 2

Ungejua jinsi gani
(If you knew how...)
Machozi lolia kwa uchungu wa penzi langu na
(The tears which were cried for the pain of my love)
Mwenzio jinsi gani, vile nimeumia moyoni
(Your friend how, the way my heart aches)
Hata kupendwa sitamani
(I don't even want to be loved)
Utamu wa mapenzi mwenzako umekula kwangu ma
(The sweetness of love, your friend, you have consumed mine)
Mwenzio sitamani, hata raha tena mi sioni
(Your friend, I don't desire it, I can't feel even comfort again)
Nasikia hivi sasa una mtoto anaitwa Mamu
(I hear that now you have a child named Mamu)
Vile akinuna mpaka tabasamu
(The way she frowns or smiles)
Mmefanana sana, sana
(You both look so similar)
Mi mwenzako tena mapenzi mi sina hamu
(Me, your friend, I have no hunger for love again)
Tena na mpango wa kuhama Dar Es Salaam
(And I plan to leave Dar Es Salaam)
Nataka niende mbali, niepuke vita na walimwengu
(I need to get far away, to escape the war and the people of this world)
Mi mwenzenu siwezi
(Me, your friend, I cannot)

Monday, September 16, 2013

Hii ndio cake ya birthday ya Ommy Dimpoz na ujumbe aliouandika kwa familia marafiki na mashabiki wake .nouma sana

Tarehe 13 / 09 ni siku ya kuzaliwa hitmaker Omari Fereji Nyembo a.k.a Ommy Dimpoz, na huu ndio ujumbe wake kwa familia,marafiki na fans wake.

I would like to thank God for the blessings he has showered me with over the years and especially during my professional musical career!! Saying Allah is great it truly an understatement. Next to him is#TeamPozKwaPoz. Mad love to my fans cause truly without you I am Nothing. Fans, family & friends, you are the pillar of my success and you are irreplaceable... Happy Birthday to ME!! And I'm thankful for everything good or bad as they all have shaped me to be the man I am today. Come celebrate life health and music with me tonight at Elements Lounge. My brothers j martins, AY and FA will be there as well making sure it's more than a birthday!! Tupogo, ama nini?!!

Happy Birthday ommy Dimpoz

Wednesday, September 11, 2013

Rich Mavoko kudondosha single mpya "Roho Yangu" wiki hii

Hit maker wa kila ngoma anayotoa Rich Mavoko, baada ya kudondosha "one time" wiki hii anatarajia kuachia mkono mwingine unaoitwa "Roho yangu" aliufanya na mazoo.

Gucci Mane achafua twitter awadiss kila mmoja unaewajua duh nouma sanaaaaaaaaa

Rapper Gucci Mane achafua twitter kwa diss ambazo amezielekeza kwa karibu kila msanii unaemfikiria. Kila mtu mwenye jina flani kutoka Atlantic Records kuanzia Nicki Minaj, Ciara, Waka, Jeezy, Rick Ross Vanessa, editor-in-chief wa XXL magazine, mpaka mschana wake mwenyewe Keyshia D’oir!....majina ni mengi fanya kuangalia mwenyewe.

Monday, September 9, 2013

KAA TAYARI NA SINGLE MPYA YA MADEE

Ikiwa bado wimbo "Sio Mimi" a.k.a Pombe Yangu unafanya vizuri sana masikioni mwa watu na hata katika shows mbali mbali anazozifanya, Madee anatarajia kudondosha mkono mwingine kutoka kwa producer Macochali, MjRecords

Hii ndio single mpya ya Ben Pol aliyoiachia katika siku yake ya kuzaliwa



Siku ya leo, tarehe 8 September ndio siku ambayo alizaliwa Bernard Paul a.k.a Ben Pol, na kwakuwa kila mmoja ana jinsi ya kusherehekea siku yake, Ben pol yeye ameamua kuachia ngoma "Waubani" akiwa
amemshirikisha msichana "Alice" ambae yeye ameamua kumpitisha kwa asilimia zote kuwa ana uwezo mkubwa wa kuimba

Wednesday, September 4, 2013

Mr Blue kuachia wimbo mpya leo MR. BLUE -PESA


Mr Blue kuachia wimbo mpya leo
Mr Blue ambaye mwaka huu ameshatoa ngoma kama “Nipende”, leo mchana anatarajia kutoa ngoma yake mpya inaitwa Pesa. Mr Blue ambaye pia ni baba wa mtoto mmoja mara nyingi amekuwa ni mtu wa kutoa wimbo mmoja na kukaa muda mrefu.

Yaliyojiri kwenye uzinduzi wa video ya wimbo mpya wa Diamond Platinum 'Number One na kumkabidhi ufunguo wa gari msanii wa zaman

Msanii wa kizazi kipya Naseeb Abdul aka Diamond Platinum jana alizindua video ya wimbo wake mpya 'Number One' kwenye hoteli ya kifahari 'Serena Hotel' iliyopo jijini Dar es Salaam.


Katika uzinduzi huo pia Diamond alimpa  zawadi ya gari Msanii Mkongwe Ngurumo aliyetangaza kustaafu siku za hivi karibuni.
Diamond alisema amesikitishwa sana baada ya kusikia msanii huyo kustaafu katika muziki na bila kumiliki gari lolote katika enzi za ujana wake mpaka uzeeni ndio sababu ya kumpa zawadi ya gari aina ya Funcargo.



Drake kumshirikisha baba yake mzazi kwenye album yake "Nothing Was The Same"

Ikiwa siku za kuachia album yake "Nothing Wa The Same" zinakaribia (Sep 24), habari zaidi zinazid kutoka. Habari zilizoenea sasa ni kuwa Drake atamshirikisha baba yake mzazi kwenye ngoma ambayo itakuwa ni bonus kwenye album hiyo " Heat of the moment."

“Naishi katika ndoto za baba yangu. Baba yangu alitaka kuwa muimbaji maarufu, kulikuwa na interview zingine ambazo waliniuliza kuhusu baba yangu, na sikutaka kuongelea kuhusu hilo, na kuna ngima ambazo sijamfanya baba yangu kuonekana ni mtu mkubwa, mwisho wa siku, baba yangu anajua kuwa nampenda na kuwa ni rafiki yangu mkubwa." amesema Drake.
Bado haijawekwa wazi kama baba mzazi wa Drake, Dennis Graham ataimba kwenye ngoma hiyo au sauti yake tu ndio itakayoskika kama sample, kama kwenye ngoma ya zamani ya Drake “Jodeci Freestyle” aliyomshirikisha J. Cole.