Thursday, October 31, 2013

Jana ilikuwa ni birthday ya mzee wa" KUKERE"Mkali Iyanya asherekea na wafungwa sema keki ndyo imezua maneno noooooma sna

Iyanya and DCP

Iyanya ambae ni staa wa Nigeria alikuja kwenye Fiesta ya juzi Dar es salaam baada ya kurudi kwao alitumia muda wake kusherekea siku yake ya kuzaliwa kwa kutembelea wafungwa, kufanya show na kuwapelekea misaada kwenye hii siku ya kutimiza miaka 27 ambapo kilicho-make headline zaidi ni keki yake.
Iyanya exiting 3
Baadhi ya ma-blogger wa Nigeria wameiita hiyo keki kama most sexiest birthday cake ever kwenye party ya star huyu ambapo manager wake Ubi Franklin pamoja na watu wake wa Man Made Music Group ndio walioandaa keki.

Iyanya exiting 4

iyanya exiting the prison 
CHECK KEKI SASA NDIO KITUKO

Iyanya's Birthday Cake 2

Tuesday, October 29, 2013

EXCLUSIVE: VIDEO YA ROMA "2030" KUTOKA TAREHE 1.11.13



Video mpya ya ROMA ambayo wengi wanaisubiria imekuwa kama gumzo hivi kwa picha zinazowekwa Instagram na Dir wa video hiyo ambaye anajulikana kwa jina la NISHER. Kila mtu anazungumza hiki wengine wanazungumza yao lakini video inatoka Ijumaa hii tarehe 1.11.13 so kaa tayari kwa kichupa hiki kikali niamini mimi ni video nzuri sana hujawahi ona

Saturday, October 26, 2013

EXCLUSIVE:NEY aliepigwa marufuku na BASATA kuvaa mlegezo.hii noooma saana


Ney wa Mitego 1

Ney wa Mitego ambae ni staa wa single za ‘muziki gani’ na ‘salamu zao’ amethibitisha kupewa barua na baraza la sanaa Tanzania ikiwa ni onyo la kutoendelea kuvaa suruali mlegezo kwenye majukwaa mbalimbali anayoonekana.
Kwenye interview yake na millardayo.com Ney amesema alipigiwa simu sana na namba moja lakini alikua amelala, alipoamka akakuta missedcalls nyingi so ikabidi apige ndio akaambiwa BASATA kuna barua yake ambapo baada ya kushindwa kwenda alipelekewa Manzese.
Ney anasema ‘sielewe kama BASATA ndio wameamua kudili na milegezo, sijaelewa wao wanaangalia nini zaidi, nimejaribu kuuliza wakasema nikiendelea watanifungia kazi zangu, ni kweli navaa mlegezo lakini kuna vitu vingi sana vya kufanyia kazi wao kama BASATA manake tunaibiwa kazi zetu kila siku mbona hawashughulikii hizo?’ mi tangu niko shule mlegezo ni tatizo langu kubwa ila nitajitahidi kupunguza japo nashangaa nimeandikiwa barua mimi mwenyewe wakati kuna wasanii wanavaa mlegezo hata kuliko mimi’

MCHIZI MOXIE kuizindua video yake "PIGA MAKOFI" siku ya birthday 1.11.2013


Ijumaa ya week ijayo tarehe 1 msanii wa Hip Hop nchini atakuwa anasherehekea siku yake yakuzaliwa pande za Hood yake Tabata. Moxie amesema mbali na kusherehekea siku yake yakuzaliwa hiyo pia anatakuwa akizindua video ke mpya kabisa inayokwenda kwa jina la PIGA MAKOFI. Ameomba ndugu jamaa na marafiki kujitokeza siku hiyo kwani kiingilio ni sawa na bure shilling elfu 5 tu na utapata BBQ bureeeeeeeee huku ukipata huduma nzuri kabisa kutoka kwa wahudumu waliobobea kwenye kazi yao hapo VIENA PUB iliyopo Tabata

Wednesday, October 23, 2013

EXCLUSIVE:DOGO JANJA HAYUPO TENA MTANASHATI

 


Janjaro msanii kutoka Arusha lakini makazi yake yapo Dar amefunguka kuwa hajafukuza na Ostaz Juma Namusoma kwenye kampuni yake ya Mtanashati bali amejitoa mwenyewe kwa hiari yake. Janjaro amesema amechoka na matendo tu ya Ostaz na alikuwa tu akiyavumilia lakini kwa sasa ameshakuwa mkubwa so nataka nikae kivyangu vyangu nifanye mambo yangu kama wasanii wengine ambao hawana meneja na wanafanya poa. Namnukuu Janjaro akisema....
 "Najua yatasemwa mengi kutoka kwa Ostaz Juma ila mimi ndio uwamuzi wangu, kuna watu wanasema sina utovu wa nidhamu lakini hao watakuwa wananijua sasa hivi hawajanifuatilia kutoka nyuma. Hata mtoto mdogo atakuwa mtundu ila akiwa mkubwa hunyooka na kuwa mtoto mzuri sasa nimekuwa mkubwa na kupelekwa pelekwa tena sitaki, kwa maelezo zaidi Ostaz Juma aongee na wazazi wangu asiongee na mimi"

INAKUJA KAA TAYARI: Captain wa Bongo Fleva soon kuachia "Msambinungwa" akiwa na Alikiba

Captain wa Bongo Fleva Tanzania, Tunda Man soon anadondonsha pini jipya  "Msambinungwa" aliyoifanya  chini ya producer Shedy Clever huku akiwa amemshirikisha Alikiba.


"Msambinungwa ni ngoma ambayo nimemshirikisha mwanangu, ndugu yangu, mnyamwezi wangu, mchizi wa geto, wengi wanamuita Alikiba au sio, ni ngoma moja kali, ngoma ya kuchezeka ngoma moja ambayo naifikiri kila mmoja ataipenda kwasababu ni kali kuliko, kaa mkao wa kula kwasababu sasa yoyote nitaidondosha ngoma hiyo Msambinungwa" amesema Tunda man

Sunday, October 20, 2013

Solo Thang kudondosha single mpya "Mdudu" ft mr.blue October 25 .Aiiiseeee

October 25,mkali wa lyrics na vina,Solo thang anatarajia kuachia historia nyingine
this time inaonekana akiwa na Mr Blue. Single inaitwa "Mdudu" kaa mkao mzuuri wa kuisikiliza. Definately is gonna be the bomb.

Saturday, October 19, 2013

BADO MASAA KWA AJILI YA KUJUA NANI KUWA MBABE.hiii noooma saaana

 

EXCLUSIVE:Check Picha na video mpya kutoka kwa Hemed PHD – Rest of my life.CHECK VIDEO CHINI



vlcsnap-2013-10-19-03h10m20s195
vlcsnap-2013-10-19-03h05m31s118
vlcsnap-2013-10-19-03h05m36s188
vlcsnap-2013-10-19-03h05m44s24
vlcsnap-2013-10-19-03h05m58s145
vlcsnap-2013-10-19-03h07m24s231
vlcsnap-2013-10-19-03h07m39s131
vlcsnap-2013-10-19-03h07m54s28
vlcsnap-2013-10-19-03h08m00s101
vlcsnap-2013-10-19-03h08m05s139
vlcsnap-2013-10-19-03h10m03s35

Alicho-post Wema Sepetu kwenye Instagram kinachomhusu Diamond platinum.aiiiiiiiiiiiise

 


Wema Sepetu mwenyewe anajua kwamba watu wengi wanafikiri yeye anawaza kuwa na Diamond hivi sasa, lakini ametoa majibu ya hayo mawazo kwenye hii picha. Maana ya hii picha ni kwamba watu wengi wanafikiri kwamba muda wote Diamond yupo kwenye kichwa cha Wema, lakini yeye mwenyewe anasema kwamba muda wote anafikiria pesa. Unaionaje hiyo picha?
wemasepetu

Thursday, October 17, 2013

EXCLUSIVE:Nay wa Mitego kuchuana na wasanii wakubwa wa Kenya na Uganda kwenye Nzumari awards.

Habari mpya kutoka kwa msanii Ney wa Mitego ni kwamba hivi sasa amepata nomination mbili kwenye category mbili tofauti katika Nzumari awards. Mwaka jana Diamond alishinda tuzo hizi na mwaka huu ni kwamba wimbo wa Ney utashinda na nyimbo za wasanii wengine wa Africa Mashariki kwenye category ya wimbo bora wa Afrika Mashariki.
Ney akiongea na millardayo.com amesema,”Nimepata nomination mbili, ya kwanza kwenye kipengele cha msanii bora wa kiume kutoka Tanzania ambapo tupo mimi,Diamond,Ommy Dimpoz na Rich Mavoko. Kipengele kingine ni wimbo bora wa Afrika mashariki ambapo nipo mimi na wimbo wa Muziki gani,Mobima wa P unit na Badilisha wa Jose Chameleone”

All the best kwenye category wimbo bora wa Afrika mashariki.

EXCLUSIVE:DAVIDO LIVE KWENYE FIESTA 2013.nooooma saaaaaanaa




Clouds Media leo hii wamethibitisha kuwaleta wasanii zaidi ya watatu kutoka nje ya Tanzania (International artist), na leo hii wamethibitisha kudondoka kwa msanii kutoka
Nigeria Davido anaefanya poa sana Africa na single kadhaa kali, ikiwemo Gobe.

CHECK HILI JARIDA LILIVYOMUANDIKA JOKATE .noooma saaanaa

Jokate 2

Hili ni Jarida jipya hapa Tanzania ambalo naambiwa Watanzania wataanza kulipata mitaani kuanzia kesho Ijumaa ila leo badae Amplifaya ya Clouds FM itafanya mpango wa kusikia kutoka kwa Jokate mwenyewe…. kaa karibu na mtu wako wa nguvu millardayo kwenye facebook, twitter na instagram kwa info zaidi.
Jokate 1

Tuesday, October 15, 2013

RIHANNA AKIWA SOUTH AFRICA KWA MADIBA



2
According to MTV BASE ni kwamba Mrembo RiRi kwenye show aliyoifanya juzi Johannesburg, inaaminika kwamba ameweka rekodi kwa kuwa msanii wa kike kupata watu wengi kwenye uwanja wa FNB Jumapili ya 13 October ambapo idadi aliyoipata ni ya zaidi ya watu elfu tisini (90)
October 16 2013 RiRi atafanya show huko Capetown South Africa ambapo wakati akiwa bado S.A ameendelea kutokelezea kwenye picha kadhaa kama hizi akiwa na Wanyama mbalimbali.
3

4

5

1

SINA TIME NA MUZIKI TENA "NOORAH BABA STYLE" NOOOMA SANA

 



Msanii wa Muda sasa kwenye Industry ya Bongo Fleva Noorah a.k.a BabaStyle amevunja ukimya kwa kuamua Kufunguka kile kilicho moyoni mwake kuhusu ukimya wake kwenye Game kwa sasa ambapo amefika mbali na kusema kuwa Mziki hauna faida kwake na kwa sasa anaufanya Mziki kama Starehe like mtu anavyotoka kwenda Bar kunywa beer huku akiwa sio Mlevi means siku akifeel ham tu.